Business

header ads

WAKADIRIAJI MAJENZI WATAKIWA KUFUATA MAADILIMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwenye wa kwanza kushoto akipata maelezo kutoka kwa Mkadiliaji majenzi .


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan mwenye ijabu akipata maelezo kutoka kwa Mkadiliaji majenzi wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Sugwa Athanas hayupo pichani alipotembelea banda hilo wakati wa uzinduzi wa mkutano wa kimataifa wa wakadiriaji majenzi Afrika uliofanyika leo jijini Dar es salaam wa kwanza kushoto ni Afisa habari wa Baraza la Taifa la Ujenzi (NCC) Bi. Roberta Makinda.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania SAMIA SULUHU HASSAN amewataka wakadiriaji majenzi nchini wahakikishe wanafanya kazi kwa kuzingatia maadili na waepuke vitendo vya rushwa katika mchakato wa ukadiriaji majengo nchini.

Makamu wa Rais Samia  Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo leo jijini Dar es Salaam wakati anafungua mkutano wa mwaka wa wakadiriaji majenzi kutoka nchini mbalimbali za Afrika ambapo amewataka wataalamu hao wakauongeza bidii katika utekelezaji wa kazi zao hasa kwa kuzingatia teknolojia za kisasa.

Amesisitiza suala la Tanzania na suala la kuhamia Makao Makuu Dodoma hivyo ni muhimu kwa wakadiriaji majenzi wakajipanga vizuri katika utekelezaji wa miradi hiyo mikubwa kwa kuweka gharama nafuu kulingana na hali halisi ya mradi unaotakiwa kujengwa.
Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN amehimiza ushirikiano kati wakadiriaji majenzi wa Tanzania na wa nchi nyingine za Afrika katika kubadilishana uzoefu kwenye kazi zao ili kuongeza ubunifu na ufanisi katika miradi wanayopata.
Kwa upande wake Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano Profesa MAKAME MBARAWA amesema serikali imetenga dola bilioni 2.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara, madaraja na bandari na viwanja wa ndege hivyo serikali inahitaji wakadiriaji majenzi waadilifu katika utekelezaji wa miradi hivyo na sio vinginevyo.
 

Post a Comment

0 Comments