Business

header ads

SERIKALI YAFUTA GHARAMA ZA KUMUONA DAKTARI KWA WAATHRIKA WA UBAKAJISerikali imefuta gharama zote za kumuona Daktari na matibabu kwa mtoto yoyote ambae atakua amebakwa au kulawitiwa ili kuhakikisha inamnusuru muathirika wa kitendo hicho na magonjwa ya kuambukiza na maumivu.Uamuzi huo umetangazwa leo Jijini Dar es salaam na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,  Jinsia, Wazee na Watoto,  Ummy Mwalimu wakati wa mapitio ya Sera ya Afya ya Mwaka 2007 yenye lengo la kuinua hali ya afya ya wananchi wote hasa walioko kwenye hatari zaidi kwa kuweka mfumo wa afya utakaokidhi mahitaji ya wananchi na kuongeza umri wa kuishi kwa Watanzania.Amesema utekelezaji wa agizo hilo umeanza kutumika mara moja na muuguzi yoyote atakayebainika anamtoza hela muathirika wa vitendo hivyo atachukuliwa hatua za kinidhamu na wananchi watoe taarifa kwa haraka kwenye maeneo husika. 

"Mzazi hana shilingi elfu 15 inambidi arudi nyumbani sasa huko ni kupoteza ushahidi, nafuta gharama zote za kumuona daktari na matibabu" alisema Ummy

Post a Comment

0 Comments