Business

header ads

RAIS SHEIN AONGOZA MAZISHI YA MZEE ABOUD JUMBE LEO

Viongozi wa kitaifa wakishiriki katika sala ya kumwombea Ras wa Awamu ya Pili wa Zanzibar, marehemu Alhaj Abood Jumbe iliyofanyika kwenye msikiti, Mwembeshauri Zanzibar Agosti 15, 2016. Kutoka kushoto ni Makamu wa Rais, Mstaafu, Dkt. Mohammed Bilal, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Aman Karume, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohammed Shein.
Wananchi waliobeba jeneza la mwili wa Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi yaliyofanyika Nyumbani kwake Migombani Unguja leo mchana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) pamoja na Viongozi mbali mbali wa Serikali ya mapinduzi na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika mazishi ya Marehemu Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi yaliyofanyika Nyumbani kwake Migombani Unguja leo mchana.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akishiriki dua maalum mbele ya jeneza lenye mwili wa marehemu Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambaye alikuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano na Rais wa Pili wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  ,nyumbani kwa marehemu Migombani Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein, amewaongoza mamia ya wananchi wa Zanzibar katika maziko ya aliyekuwa rais wa pili wa Zanzibar, Aboud Jumbe Mwinyi aliyefariki dunia jana nyumbani kwake jijini Dar es salaam.

Maziko hayo yamefanyika katika Makaburi ya Migombani Unguja, na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali, wakiwemo wastaafu wa ngazi mbalimbali pamoja na wanasiasa wa Tanzania bara na visiwani.

Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan,Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, rais mstaafu wa awamu ya pili wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi, rais mstaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume na aliyekuwa Makamu wa Kwanza wa Rais katika serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Zanzibar Maalim Seif Hamad.

Akimuelezea marehemu, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan amemwelezea marehemu Aboud Jumbe Mwinyi kama kiongozi ambaye aliitetea demokrasia pamoja na kufanya kazi kwa wazanzibari kwa kuimarisha umoja na mshikamano.

Post a Comment

0 Comments