Business

header ads

RAIS DKT JOHN POMBE MAGUFULI APOKEA HATI ZA UTAMBULISHO KUTOKA KWA MABALOZI1 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Canada Mhe Ian Myles Ikulu jijini Dar es salaam agosti 24, 2016
2

3 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Canada Mhe Ian Myles Ikulu jijini Dar es salaam agosti 24, 2016
4 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Thailand hapa nchini Mhe. Prasottiporn Wetpraisait Ikulu jijini Dar es salaam agosti 24, 2016
5 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Thailand hapa nchini Mhe. Prasottiporn Wetpraisait Ikulu jijini Dar es salaam agosti 24, 2016
6 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akipokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Austria hapa nchini Mhe. Harald Gunther Ikulu jijini Dar es salaam agosti 24, 2016
7Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli katika mazungumzo baada ya kupokea hati ya utambulisho toka kwa Balozi wa Austria hapa nchini Mhe. Harald Gunther Ikulu jijini Dar es salaam agosti 24, 2016Rais Magufuli amepokea hati za utambulisho kutoka kwa mabalozi watatu wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini.

Mabalozi waliowasilisha hati zao ni Mhe. Ian Myles - Balozi wa Canada hapa nchini, Mhe. Prasittiporn Wetprasit - Balozi wa Thailand hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi nchini Kenya na Mhe. Harald Gunther - Balozi wa Austria hapa nchini mwenye makazi yake Mjini Nairobi nchini Kenya.

Pamoja na kuwasilisha hati zao za utambulisho Mabalozi hao wameelezea kufurahishwa na mahusiano na ushirikiano mzuri uliopo kati ya nchi zao na Tanzania na wameahidi kufanya kazi bega kwa bega na Serikali ya Tanzania ili wananchi wa pande zote wanufaike na matokeo ya ushirikiano huo hususani katika uwekezaji na biashara.

Kwa upande wake Rais Magufuli amewahakikishia Mabalozi hao kuwa Serikali ya itaendeleza na kukuza zaidi ushirikiano kati ya Tanzania na nchi hizo na ametoa wito kwa Mabalozi hao kuzishawishi zaidi nchi zao na wawekezaji katika nchi hizo kushirikiana na Tanzania katika ujenzi wa viwanda, uongezaji thamani ya madini, kuendeleza kilimo hususani kilimo cha umwagiliaji, uzalishaji wa nishati na biashara mbalimbali.

Pia Rais Magufuli ametoa wito kwa Mabalozi wa Thailand na Austria kuanzisha ofisi za Ubalozi hapa nchini ili kurahisisha na kuharakisha shughuli za kibalozi.  


Post a Comment

0 Comments