Business

header ads

NBS YAPOKEA MSAADA WA BIL.25 KUSAIDIA WATOTONaibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akionyesha Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania mbele ya wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa taarifa hiyo jijini Dar es salaam.


Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji akiongea mbele ya wadau mbalimbali wa takwimu hawapo pichani wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania jijini Dar es salaam.


Wadau mbalimbali wa takwimu wakimsikiliza Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji hayupo pichani wakati wa uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania jijini Dar es salaam.Habari/Picha Na Ally Daud 
Tume ya Taifa ya Twakimu (NBS) imepokea msaada wa shilingi bilioni 25 kutoka Umoja wa Ulaya kwa ajili ya kusaidia kuboresha tasnia ya takwimu kuhusu haki za watoto nchini.

Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa Taarifa ya Hali ya Umaskini wa Watoto wa Tanzania Naibu Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Ashatu Kijaji amesema kuwa amepokea msaada huo kwa nia ya kuendeleza tasnia ya takwimu nchini na kusaidia malengo ya nchi ya miaka mitano.

“Tumepokea msaada huu kwa furaha na hamasa kubwa katika kufikia lengo letu la kuboresha na kukuza tasnia ya takwimu nchini ili kuweza kupata taarifa muhimu kwa ajili ya maendeleo ya miaka mitano ya nchi yetu”. Alisema Mhe. Kijaji.

Aidha Mhe. Kijaji amesema kuwa Wizara yake imewapa kipaumbele watoto kwa kutenga shilingi. Bilioni 18 kila mwezi ili kuwasaidia katika mambo  muhimu ya kila siku hususani elimu bora, makazi na malazi.

Mbali na hayo Mhe. Kijaji ameshukuru na kuwapongeza Umoja wa ulaya kwa msaada huo na kuwataka wasichoke kuwa nao pamoja katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030.

Kwa upande wa Mwakilishi wa Balozi wa Umoja wa Ulaya Bw. Eric Beaume  Amesema kuwa msaada huo sio mwisho wao kwani wanapenda kazi ya NBS na matokeo yake hivyo wapo tayari kutoa kiasi kikubwa zaidi ili kuwezesha tume hiyo kutoa takwimu zenye uhakika kwa maendeleo ya Tanzania.

Bw.Beaume amesema kuwa Umoja wao utakua bega kwa bega na Tanzania katika kutoa misaada ili kusaidia haki zote za watoto ili kujenga taifa lenye tija na muamko wa kimaendeleo kutokana na takwimu zitokanazo na tume hiyo.

Aidha Bw. Beaume ameongeza kuwa Umoja wao upo tayari kusaidia Nyanja za kilimo, Nishati katika maeneo ya vijijini ili kuunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu kwa miaka mitano ijayo.

Mbali na hayo Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa amesema  kutokana na msaada huo wamepata hamasa kubwa kwa tume hiyo kuweza kupambana na kupata takwimu yakinifu zitazopelekea kuleta ufumbuzi wa matatizo mbalimbali yahusuyo jamii nchini na kufikia malengo ya miaka mitano.

Post a Comment

0 Comments