Business

header ads

MWENYEKITI WA BODI YA PAROLE APIGA MARUFUKU SUNGUSUNGU KUKAMATA DADA POAMwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema akisisitiza jambo kwa wananchi wa Mtaa wa Pakacha kata ya Tandale Uwanja wa Fisi wakati alipokwenda kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi hao hasa akina mama.
Mjumbe wa Bodi ya Parole Bi. teddy Killa akizungumza na wananchi wa Mtaa wa Pakacha kata ya Tandale Uwanja wa Fisi wakati Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Augustine Mrema alipokwenda kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi hao hasa akina mama, 
Wanancihi wa Mtaa wa Pakacha kata ya Tandale Uwanja wa Fisi wakimsikiliza kwa makini Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema (hayupo pichani) wakati alipokwenda kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi hao hasa akina mama.
Mwenyekiti wa Mtaa wa Pakacha kata ya Tandale Uwanja wa Fisi akimkaribisha Mgeni Rasmi Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema wakati alipokwenda kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi hao hasa akina mama.
Msoma Risala kwa niaba ya wakazi wa Mtaa wa Pakacha kata ya Tandale Uwanja wa Fisi Bi. Thabita Julius (katikati) akisoma risala wakati Mwenyekiti wa Bodi hiyo Dkt. Augustine Mrema alipokwenda kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wakazi hao hasa akina mama.
Mmoja ya wakazi wa Mtaa wa Pakacha kata ya Tandale Uwanja wa Fisi ambaye jina lake halikupatikana akimueleza Mwenyekiti wa Bodi ya Parole Dkt. Augustine Mrema (hayupo picha) kero mbalimbali zinazowakabili hasa akina mama wakati Mwenyekiti huyo alipowatembelea mapema hii leo.

Mwenyekiti wa bodi ya Parole nchini Tanzania Bw. Augustino Mrema amepiga marufuku walinzi shirikishi na sungusungu kuwakamata wasichana katika maeneo ya Manzese na Tandale kwa madai kwamba wanafanya biashara ya kuuza miili yao.

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo leo jijini Dar es salaam, Mrema amehoji uhalali wa kuwakamata wasichana hao bila ya kuwakamata wanaume wanaokwenda kununua biashara hiyo jambo ambalo amesema ni kuwaonea na ni uzalilishaji kwao.

Nao baadhi ya wasichana walioongea na kurasa wamemshukuru mwenyekiti huyo wa bodi ya Parole kwa hatua hiyo na kusema kwamba wamekuwa wakipata shida ya kukamatwa mara kwa mara na kutakiwa kutoa pesa ili waachiwe.
 

Post a Comment

0 Comments