Business

header ads

MSAADA WA BILIONI 142.23 KUBORSHA VITUO VYA AFYA TANZANIAKatibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya akiongea na wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini hawapo pichani wakati wa kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo vya afya nchini


Wadau wa Nchi washiriki kutoka Canada,Uswizi, Denmark na Korea kusini wakiwa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya katikati mara baada ya kusaini msaada wa Bilioni 142.23 kwa ajili ya kuinua vituo vya afya nchini.
 Habari/Picha Na Ally Daud

Serikali chini ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto imepokea msaada wa shilingi bilioni 142.23 kutoka  nchi washiriki Canada, Denmark, Uswizi na Korea Kusini ili kusaidia kuinua vituo vya afya nchini.


Akizungumza mara baada ya kusaini msaada huo Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia ,Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisabisya amesema kuwa msaada huo wataupeleka moja kwa moja katika Zahanati za vijiji,Hospitali za  Wilaya na mkoa ikiwa pamoja na vituo vya afya nchi nzima.

“Tumepokea msaada huo kwa furaha kubwa na kuhaidi kupeleka fedha hizo hizo mahali panapohitajika kwa matumizi ya kukuza na kuboresha vituo vya afya katika zahanati na hospitali nchi nzima ili kuokoa maisha ya watanzania” alisema Dkt. Ulisabisya.

Aidha Dkt. Ulisabisya anaishukuru Benki ya Dunia kwa kuimarisha na kusaidia mfuko wa maendeleo ya afya nchini kwa kuwakutanisha na wahisani kutoka nchi mbalimbali.

Mbali na hayo Dkt.Ulisabisya amewaomba Benki ya Dunia na nchi wahisani wasichoke na kushindwa kuisaidia Tanzania katika sekta ya Afya ili kutokomeza maradhi kwa kiwango kikubwa  na kupambana kwa ajili ya kukuza uchumi wa nchi.


Post a Comment

0 Comments