Business

header ads

MAANDAMANO YA UKUTA YAAHIRISHWA KWA MWEZI MMOJA Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimeahirisha Maandamano ya Umoja wa Kupinga Udikteta (Ukuta), yaliyopangwa kufanyika kesho kwa kile walichodai ni kusikiliza na kuheshimu maoni ya wadau wakiwamo viongozi wa dini.

Akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari, Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe alisema chama hicho kinatambua haki za chama hicho lakini kinatambua zaidi haki za wananchi za kuishi.

“Tunatambua mchango mkubwa uliotolewa na wananchi na viongozi katika kuilinda Amani yetu, sisi tunawaheshimu viongozi wetu, tumekutana nao na kusikiliza ushauri wao wa kuahirisha Ukuta kwa wiki mbili au tatu,” alisema

Alisema maombi ya viongozi wa dini ni ya busara na kwa sababu hizo, Chadema kinachukua fursa hiyo kuwatangazia viongozi wa Chadema ,watanzania na wafuasi wa chama hicho kuahirisha maandamano hayo ili kutoa nafasi kwa viongozi wa kiroho kukutana na Rais ili kutafuta suluhu ya jambo hilo.
Post a Comment

0 Comments