Business

header ads

KINGUNGE AOMBA RAIS KUWAITA VIONGOZI WA CHADEMAAliyekuwa kada wa CCM, Kingunge Ngombale Mwiru amewaomba marais wastaafu, Rais Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa kuzungumza na Rais John Magufuli ili aitishe kikao kati ya Serikali na Chadema kwa ajili ya kusitisha maandamano yaliyopangwa kufanyika Septemba Mosi.

Kada huyo ambaye alijivua uanachama wa CCM Oktoba mwaka jana kwa madai kwamba chama hicho kinaendeshwa kwa maslahi binafsi, amesema kuwa mazungumzo hayo yataepusha uvunjifu wa amani nchini.

Kingunge ambaye ameomba kwenye jopo hilo wawepo mawaziri wakuu wastaafu, Edward Lowassa na Fredrick Sumaye na wanapaswa kutambua wajibu wao kwa Watanzania na kwamba hawapaswi kukaa kimya wakati hali kama hiyo inaendelea nchini.

Post a Comment

0 Comments