Business

header ads

JITIHADA ZA KUIFIKISHA TANZANIA YA VIWANDA ZAANZA

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ushonaji wa suruali za Jeans wakati alipotembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agosti 10, 2016.  Kulia kwake ni Katibu Mkuu wa  Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dr. Adelhem Meru na wapili kushoto ni Meneja Mkuu Msaidizi wa kiwanda hicho, Rigobert Massawe.

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza  baada ya kutembelea kiwanda cha kushona nguo cha Tooku kilichopo kwenye eneo la EPZ, Mabibo External jijini Dar es salaam Agost 10, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa kiwanda cha kushona nguo cha  Tooku kilichopo eneo la EPZ,Mabibo External jijini Dar es salaam baada ya kutembelea kiwanda hicho na kuzungumza, Agosti 10,2016.  Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Dkt. Adelhem Meru na kulia kwake ni Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing. 
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu,  Mh. Majaliwa Kassim Majaliwa, amesema jitihada za kuifikisha Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati kupitia ujenzi wa viwanda zimeanza kuzaa matunda baada ya baadhi ya viwanda vilivyojengwa nchini kuanza kuuza bidhaa katika masoko ya kimataifa na kutoa fursa ya ajira kwa idadi kubwa ya Watanzania.

Mh. Majaliwa amesema hayo leo alipotembelea kiwanda kinachimilikiwa na Wachina cha Tooku Garment Company Limited kilichopo eneo la Mabibo External jijini Dar es Salaam, ambapo akiwa kiwandani hapo Waziri Mkuu ameoneshwa jinsi uzalishaji unavyofanyika huku vijana mia nne wakipatiwa mafunzo na kuajiriwa kila mwezi, lengo likiwa ni kuajiri Watanzania elfu sita katika kipindi kifupi kijacho.

Aidha, Waziri Mkuu amesema uwepo wa kiwanda hicho utachochea thamani ya mazao ya kilimo hususani soko la pamba, kwani nguo zinazotengenezwa na kiwanda hicho ni za daraja la kwanza na zenye soko kubwa nchini Marekani ambazo pia zinakidhi mahitaji ya soko la ndani.

Post a Comment

0 Comments