Business

header ads

JESHI LA POLISI DAR LAPINGA MAANDAMANO


 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha magazine ya kuwekea risasi zilizokamatwa jijini Dar es Salaam.

 Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha site Mirror zilizoibwa katika magari leo jijini Dar es Salaam.
Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishina Simon Sirro akionyesha flana rangi mbalimbali zilizokamatwa. 
(Picha na MICHUZI BLOG)Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano yoyote yenye lengo la kuvunja amani pamoja na kukataza kusambazwa kwa fulana zilizoandikwa neno Ukuta, ambalo linalenga kuhamasisha maandamano ya Ukuta.


Akiongea na waandishi wa habari wakati akiwasilisha taarifa ya kukamatwa kwa majambazi 3, magazine 10 na risasi 300 kamanda wa kanda Maaluma ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Siro, amewata wanachama wa Chadema kutii sheria bila shuruti kwani maandamano hayo waliopanga kuyafanya Septemba Mosi jeshi hilo halitoyaruhusu kufanyika.

Mbali na agizo hilo, jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata majambazi watatu katika matukio tofauti na risasi 300 pamoja na mwizi wa magari ambapo uchunguzi wa makosa yao unafanyika na baadaye kufikishwa mahakamai.

Aidha, jeshi linaendelea na upepelezi wa kumbaini kijana mmoja aliyefanikiwa kulipua bomu kwa polisi jamii wa eneo la Mabibo Loyola Jijini dar es Salaam na kufanikiwa kukimbia kusiko julikana.
 
Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Agasti 20 majira ya saa 12:00 jioni lilipata taarifa toka kwa raia wema kuwa maeneo ya mtaa wa Ufipa Kinondoni kuna duka linauza flana rangi mbalimbali zenye maneno ya uchochezi yaliyoandikwa ‘’TUJIPANGE TUKATAE UDIKITETA UCHWARA’’ rangi nyeupe idadi yake 28, rangi nyekundu fulana 18 zenye  maneno ‘UKUTA’ fulana 6  za Kakhi zenye maneno ‘’UKUTA’ Na fulana zingine rangi nyeusi 23 zenye maneno ’’UKUTA’’. 

Aidha Polisi baada ya kupata taarifa hizo walifika eneo la tukio na kumkamata mtuhumiwa Yoram Sethy Mbyelllah (42) mfanyabiashara, mkazi wa Mburahati akiwa anauza fulana hizo dukani kwake. Mtuhumiwa anaendelea kuhojiwa na baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani.

Post a Comment

0 Comments