Business

header ads

BEI YA PETROL YAPANDA 0.88%Mamlaka ya udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji(EWURA), imetangaza kupanda kwa beo ya mafuta kuanzia hii leo kutokana na mabadiliko ya bei katika soko la Dunia.


Akioongea na Waandishi wa Habari jana Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa (EWURA), Bw. Felix Ngamlagosi amesema kuwa bei hizo za jumla na reja reja zimepanda kwa aina zote za mafuta ya Petroli Dizeli na ya taa.


Ngamlagosi amesema kuwa be za reja reja,zimeongezeka kwa shilingi 17 kwa lita moja ya petroli sawa na asilimia 0.88,dizeli sh.90 kwa lita sawa na asilimia 5.24 na mafuta ya taa sh.72 kwa lita sawa na asilimia 4.28 ikilinganishwa na bei ilitangazwa kipindi kilichopita.


Mkurugenzi huyo amtoa ufafanuzi juu ya kuongezeka kwa bei hiyo na kusema kuwa kuongezeka huko kwa soko la ndani kumetokana na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia na gharama za usafirishaji wa bidhaa hiyo kuja nchini.Pamoja na mabadiliko hayo ynayohusu nchini nzima lakini amesema mabadiliko hayo hayatabadilika katika mkoa wa Tanga ambapo vituo vvya mafuta mkoani humo vimeagizwa kutokupandisha bei ya mafuta.

Post a Comment

0 Comments