Business

header ads

URENO YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA ULAYA


Ureno imekuwa timu ya kwanza kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Poland kwa changamoto ya mikwaju ya penati 5-3 baada kumaliza mchezo kwa sare ya bao 1-1.

Mpambano ulianza kwa kasi sana, mpira mrefu uliopigwa na beki wa kulia wa Poland Piszczek unamfikia Maczynski wingi ya kushoto naye bila ajizi anampelekea Lewandowski ambaye bila ajizi anaukwamisha mpira huo kimiani, hii ni dakika ya pili tu ya mchezo.
Baada ya hapo mashambulizi yanakuwa kwa pande zote mbili lakini kunako dakika ya 32 pasi safi ya kisigino toka kwa Nani inamkuta Renarto anayefunga kwa shuti kali la mguu wa kushoto na kuipatia Ureno bao la kusawazisha.Hadi kipindi cha kwanza kinamalizika bao lilikuwa 1-1.

Dakika 45 za kipindi cha pili hakikuwa na mabadiliko yoyote zaidi ya timu zote kushambuliana kwa zamu huku Ronaldo kwa upande wa Ureno na Lewandowski kwa upande wa Poland wakionesha umahiri wao ila bahati haikuwa yao kwani walikosa magoli mengi.
Muda wa nyongeza (extra time) zilikwisha kama zilivyomalizika dakika 90,hivyo ikabidi mshindi apatikane kwa miguu 12 ya mtu mzima yaani mikwaju ya penati, ndipo Ronaldo,Renarto,Moutinho,Nani na Quaresma walipoifungia Ureno penati zote 5 na Lewandowski,Milk na Glik wakipata kwa upande wa Poland,aliyekosa ni Blaszczykowski.

Post a Comment

0 Comments