Business

header ads

SERIKALI YATAKA WANANCHI KUHESHIMU TUNU ZA TAIFAMpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bw. Kassian Chibogoyo (katikati) akionesha kwa waandishi wa habari (hawapo pichani)  baadhi ya vielelezo sahihi vya Taifa vinavyotakiwa kutumiwa na wananchi wakati alipokuwa akielezea umuhimu wa wananchi kutumia vielelezo sahihi vya Taifa


Serikali imetoa mwezi mmoja kwa wanaogushi nyaraka za serikali kuacha mara moja kwani ni kinyume na sheria

Uamuzi huo umetangazwa jijini  Dar es Salaam na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali, Bw.  Chibogoyo Cassian wakati akitoa maelekezo ya matumizi sahihi ya vielelezo  vya taifa na kutoa mwezi mmoja kwa wanaogushi nyaraka za serikali kuacha na kuwa watachukuliwa hatua za kisheria kwa atakayebainika.

Aidha amewata watendaji wa Serikali Kuu, taasisi na halmashauri za Serikali za Mitaa kuhakikisha wanakuwa na bendera ya Tanzania na bendera ya Afrika Mashariki pamoja na kubadilisha bendera zote zilizopauka na kuchanika

Bw. Chibogoyo amesema amesema kuwa wakati sasa umefika kwa jamii kuendeleza utamaduni uliokuwapo wa kuheshimu na kufuata desturi zilizowekwa katika kuendeleza umoja, amani na mshikamano.

‘Natoa wito kwa watanzania wote, katika kufanya maboresho ya kurejesha hadhi ya taifa tunapaswa kuheshimu sana Vielelezo vya Taifa letu, hapa na maanisha tuheshimu wimbo wa taifa na Nembo ya Taifa.’

Amesema kuwa katika kuhakikisha vielelezo hivyo vinaheshimiwa Ofisi yake imejipanga kufuatilia kwa karibu wale wote watakao kiuka matumizi sahihi ya Vielelezo vya Taifa ikiwemo Nembo, Bendera na Wimbo wa Taifa.

Aliongeza kuwa kuanzia sasa matumizi ya Bendera ya Taifa yatakwenda sambamba na matumizi ya Bendera ya Jumuiya ya Afrika Mashariki hivyo amezitaka Ofisi zote za Serikali pamoja na Taasisi zake waanze utaratibu wa kupandisha pia bendera hiyo kwani Tanzania tunaamini katika ushirikiano huo.

Post a Comment

0 Comments