Business

header ads

HALMASHAURI KUU YA TAIFA YA CCM YAPITISHA JINA LA DKT MAGUFULI Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula na wapili kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete akisisitiza jambo mbele ya Wajumbe wa Mutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodoma Julai 21, 2016.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha  Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete kufungua Mkutano wa Halmashauri Kuu ya taifa ya CCM mjini Dodomam leo Julai 21, 2016. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mtarajiwa, Rais John Pombe Magufuli na Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Rais wa Zanzibar Dkt, Ali Mohamed Shein . Kulia ni Makamu Mwenye kiti wa CCM, Bara, Philip Mangula . 
 Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Makamu wa Rais, Samia Suluhu na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakiimba  wimbo wa CCM katika kikao cha  Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM kilichofanyika mjini Dodoma Julai 21, 2016.
  Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakiwakaribisha viongozi wa Meza Kuu,mara walipokuwa wakiingia ukumbini wakiongozwa na Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete 
 Baadhi ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete wakati alipofungua mkutano wao mjini Dodoma Julai 21, 2016.
HABARI KAMILI
Kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimelipitisha kwa kauli moja jina Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk, John Magufuli kuwa mgombea wa uenyekiti wa chama hicho akimrithi mtangulizi wake Jakaya Mrisho Kikwete.

Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya CCM mjini Dodoma, Msemaji wa Chama Cha Mapinduzi, Christopher Ole Sendeka amesema kuwa baada ya NEC kupitisha jina hilo ni wajibu wa Halmashauri kuu ya Taifa kuwasilisha jina hilo kwenye mkutano mkuu wa CCM utakaofanyika kesho kwenye ukumbi wa mpya wa CCM.
Ole Sendeka amesema kuwa ana imani na wajumbe wote wa mkutano Mkuu maalum wa CCM kuwa watampa kura za kutosha Dk, Magufuli kuwa mwenyekiti wa tano wa CCM tangu kuanzishwa kwake.

Awali akifungua kikao cha NEC Mwenyekiti wa CCM Dk, Jakaya Kikwete amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kiko imara na kwamba kama hakikuvunjika mwaka 2015 hakitavunjika tena kutokana na mgawanyiko wa wanachama uliokuwepo katika kupata jina la mgombea urais kupitia chama hicho.

Post a Comment

0 Comments