Business

header ads

BARAZA LA MITIHANI TANZANIA LATANGAZA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2016Baraza la mitihani la Tanzania (NECTA) leo limetangaza matokeo ya mtihani wa kidato cha sita ulofanyika mwezi may mwaka huu ambapo kiwango cha ufaulu kwama mwaka 2016 ni asilimia 97.32 ikilinganmishwa na asilimia 98.65 mwaka 2015.
Akitoa matokeo hayo mbele ya waandishi wa habari katibu mtendaji wa baraza hilo Bw. Charles Msonde ameeleza kuwa licha ya ufaulu kushuka lakini kiwango cha ubora wa watanhiniwa katika madaraja ya ufaulu imeongezeka.
Bw. Msonde amesema kati ya watahiniwa 74,896 waliosajiliwa kufanya mtihani wa kidato cha sita watahiniwa 956 hawakufanya mtihani , wavulana walifaulu ni 39,466 sawa na asilimia 97.55 na wasichana waliofaulu ni 24,062 sawa na asilimia 98.59.

Aidha amezitaja shule iliyoshika nafasi ya kwanza ni Shule ya sekondari ya Kisimiri kutoka mkoa wa Arusha huku shule ya mwisho kitaifa ikiwa ni shule ya sekondari ya Lumumba iliyopo katika mkoa wa Unguja.

Idadi ya watahiniwa wa kujitegemea waliofaulu mtihani ni 8,023 sawa na asilimia 92.64 ikilinganishwa na mwaka  2015 watahiniwa wa kujitegemea walikuwa 4,076 sawa na asilimia 88.34 waliofaulu mtihani huo.

Msonde ameeleza kuwa ikilinganishwa na mwaka 2015, takwimu za ufaulu kimasomo zinaonesha kushuka kwa ufaulu, katika masomo ya sayansi kati ya asilimia 5.36 na 8.9, kwa upande wa  masomo ya sanaa kati ya asilimia 0.00 na 4.43 na masomo ya biashara kati ya asilimia 1.7 na 6.9.
Baraza la mitihani Tanzania limetoa 
Matokeo ya kidato cha sita (ACSEE) na ualimu (DSEE na GATCE) 2016 leo.


Post a Comment

0 Comments