Business

header ads

ASKARI ALIYEHUSIKA NA KIFO CHA MWANGOSI ATUPWA JELA MIAKA 15

Mjane wa marehemu Daudi Mwangosi Itika Mwangosi (kulia) akifurahia jambo na ndugu yake mzee Marko Mfugale mahakamani hapo leo.

MAHAKAMA kuu ya Tanzania kanda ya Iringa imemhukumu kwenda jela miaka 15 askari Polisi Kikosi cha Kutuliza Ghasia ( FFU ) Iringa namba G 58 Pacificius Cleophace Simon (27) kwa kosa la kumuua bila kukusudia mwanahabari Daudi Mwangosi mwaka 2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi, wakati akiwa katika majukumu yake ya kikazi. 
Akisoma hukumu hiyo, Jaji Dkt. Paul Kihwelo, alisema kuwa mshitakiwa amekutwa na hatia hiyo ya kuua bila kukusudia katika shitaka la pili lililosomwa Mahakamani hapo hii leo, baada ya shitaka la kwanza kusomwa na kukutwa hana hatia.

Kesi hiyo ilianza kusikilizwa mwezi Februari 12, 2015, na kufikia hukumu hiyo ya kumtia hatiani hii leo. Tukio hilo lilitokea 2/9/2012 katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi, Mkoa wa Iringa.
Deogratus Nsokolo ni Rais wa Club za wandishi wa habari Tanzania na Deodatus  Balile ni makamu mwenyekiti jukwaa la wahariri Tanzania wamesema pamoja na mahakama kutenda haki katika kesi hiyo lakini changamoto kubwa ipo kwa jeshi la polisi ambalo limekuwa likitumika kunyima uhuru kwa wanahabari kufanya kazi zao hali ambayo inadaiwa kuwa siyo ya kawaida.


Rais wa umoja wa klabu za waandishi wa habari Tanzania Bw Deo Nsokolo akizungumza na wanahabari baada ya hukumu ya kesi hiyo.
Picha na Francis Godwin, Iringa.

Post a Comment

0 Comments