Business

header ads

WABUNGE WAWILI CHADEMA WASIMAMISHWA VIKAO VITANO


 MBUNGE WA VITI MAALUMU CHADEMA SUZAN LYMO PICHANI (KULIA)
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania limeawasimamisha wabunge wawili wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Suzan Lymo na Mhe. Anatrophia Theonest kutohudhuria vikao vya bunge visivyozidi vitano kwa kusema uongo bungeni.

Uamuzi huo umetolewa leo na Kiti cha Spika baada ya mapendekezo ya Kamati ya Bunge ya Haki, Maadili na Madaraka ya bunge kupendekeza kuwa wabunge hao wapewe adhabu hiyo baada ya kubainika ni kweli waliliambia bunge uongo kwa nyakati tofauti..

Akisoma mapendekezo hayo Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge Mhe. Almas Mahige amesema kuwa wabunge hao walidanganya bunge kwa kuwashutumu Mhe. Hamad Yusuf Masauni aliyeshutumiwa na Mhe. Suzan Lyimo, pamoja Mhe.William Lukuvi aliyeshutumiwa na Mhe. Anatrophia Theonest ambapo wote kamati imebaini walisema uongo..

Post a Comment

0 Comments