Business

header ads

MABAKI YA NDEGE YA EGYPT AIR YAPATIKANAMabaki ya ndege iliyopotea katika bahari ya  Mediteranian mwezi uliopita  yametajwa kupatikana , Wapelelezi wa Misri wamesema.

Kikosi kinachotafuta mabaki ya ndege hiyo kimesema kimepata baadhi ya mabaki hayo katika bahari ya Mediterranian.

Kifaa kilichozamishwa katika kina cha bahari kimetoa picha ya kwanza kuhusiana na mabaki ya ndege hiyo.

Ndege hiyo aina ya Airbus A320  iliyokuwa na abiria 66 ilipotea mwezi Mei ikitokea Paris Ufaransa kwenda Cairo Misri baada ya kupoteza mawasiliano na vituo vya uongozaji vya Ugiriki na Misri kabla ya kutoweka angani.

Post a Comment

0 Comments