Business

header ads

HIFADHI KUBWA YA GESI YA HELIUM YAGUNDULIWA TANZANIAWatafiti kutoka nchini Uingereza wamegundua hifadhi kubwa zaidi duniani ya gesi adimu zaidi ya Helium katika mkoa wa Mtwara nchini Tanzania.

Watafiti kutoka chuo kikuu cha Oxford na kile cha Durham kwa ushirikiano na wataalumu wa madini kutoka Norway wamegundua uwepo wa takriban futi bilioni 54 za gesi hiyo ya barafu kama inavyofahamika Ugunduzi uliofanyika katika eneo la bonde la ufa la Tanzania.

Katika taarifa kwa wanahabri huko Japan, watafiti hao wanasema kuwa uhaba wa gesi hiyo kote duniani ulikuwa umesababisha taharuki haswa kwa madaktari ambao wanatumia gesi hiyo adimu kuendesha mashine za utabibu zijulikanazo kama MRI scanners, mbali na kutumika katika mitambo ya kinyuklia .

Nchi ya Tanzania inatajwa kuwa ni miongoni mwa mataifa chache duniani yaliyojaliwa kuwa na rasilimali na madini mengi.Kabla ugunduzi huo watafiti walikuwa wamebashiri ukosefu wa gesi hiyo baridi ifikapo mwaka wa 2035.

Post a Comment

0 Comments