Business

header ads

WACHINA WAHUKUMIWA MIAKA 30 JELA Raia wa Kichina kutoka kulia ni na Xu Fujie na  Huang Jing  ambao wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 jela au kulipa faini ya shilingi bilioni 54 leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
 Raia wa kichina wakisindikizwa na Askari Magereza mara baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka 30 jela leo katika mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii.

Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Raia wa China wawili wamehukumiwa kifungo cha miaka 30 au kulipa zaidi ya sh.bilioni 54 kila mmoja kwa kukutwa na hatia ya makosa mawili.

Washitakiwa hao katika kosa la kwanza ni kukutwa ni kuwa na nyara ya serikali ya vipande vya meno ya tembo 706 yenye thamani ya zaidi ya sh.bilioni tano na kosa la pili kushawishi kutoa rushwa kwa askari sh.milioni 30.

Washitakiwa hao ni Huang Jing pamoja na Xu Fujie wameanza kutumikia kifungo hicho leo baada ya kushindwa kutoa faini hiyo.

Akisoma hukumu hiyo Hakimu         Mfawidhi wa Mahakama ya Kisutu, Sprian Mkeya amesema kuwa kutokana na kupata maelezo katika pande zote mbili pamoja na kuisababishia hasara serikali washitakiwa adhabu yao ni miaka 30 au kulipa  ya zaidi ya bilioni tano (5).

Hakimu Mkeya amesema washitakiwa hao wanaweza kukata rufaa makahakama kuu kutokana na hukumu iliyotoka.

Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi aliomba mahakama iwape adhabu kali kutokana na kosa waliolifanya na kudai kuwa kutokana na kukamatwa kwao vitendo vya uhalifu kwa wanyamapori vimepungua
Kwa upande wa Wakili upande wa washitakiwa Nehemia Mkoko aliomba mahakama kuwaonea huruma kwa adhabu wataoipata ili waweze kutoka na kuweza kujumuika na familia zao. Washitakiwa hao walikamatwa 2010 katika eneo la mikocheni mwaka huu.
SOURCE: MICHUZI

Post a Comment

0 Comments