Business

header ads

RAIS WA VIETNAM KUFANYA ZIARA TANZANIAWaziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustine Mahiga (Mb.) (kulia), akizungumza na Waandishi wa Habari kuhusu ziara ya kitaifa ya siku 4 ya Rais wa Vietnam nchini, Mhe.Truong Tan Seng kuanzia tarehe 08 hadi 11 Machi, 2016. Ziara hiyo itakuwa ni ziara ya kwanza ya kuja Tanzania pia Afrika. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali, Bi. Mindi Kasiga naye akisikiliza kwa makini mazungumzo ya Waziri na Waandishi wa Habari.

Waandishi wa Habari wakimsikiliza kwa makini Balozi Mahiga (hayupo pichani). 
Rais wa Vietnam Bw. Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara ya siku tatu nchini Tanzania kuanzia tarehe 8 ya mwezi huu ambapo akiwa nchini anatarajiwa kusaini mikataba mbali mbali ya kibiashara pamoja na kuona fursa za uwekezaji.

Waziri wa mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kikanda na Kimataifa Balozi Augustin Mahige amesema hayo leo jijini Dar es salaam wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari huku akibainisha namna Tanzania itakavyonufaika na ziara hiyo.Post a Comment

0 Comments