Business

header ads

RAIS MAGUFULI AMTEUA DKT.RIOBA KUWA MKURUGENZI TBC


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa watendaji wakuu wa Taasisi tatu za serikali kwa mujibu wa mamlaka aliyonayo. 

Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambae anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na 

Dkt. Ramadhan Dau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi. Pia, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) ambae anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Clement Mshana ambaye amestaafu. 

Aidha, Rais Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Dkt. Mussa Iddi Mgwatu kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) ambae anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.

Post a Comment

0 Comments