Business

header ads

MAKAMU WA RAIS AAHIDI SERIKALI KUENDELEA KUTOA FURSA ZA UONGOZI KWA WANAWAKE


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza wakati wa kuzindua Programe maalum ya Mwanamke na wakati ujao (Female Future) ambayo itawajengea uwezo wanawake katika bodi za wakurugenzi wa taasisi na makampuni mbalimbali iliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Hyatt Regency  jijini Dar es Salaam leo.
Makamu Mwenyekiti wa kampuni ya ATE, Zuhura Muro akizungumza na wanawake kutoka kutoka makampuni mbalimbali leo wakati Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizindua mpango malumu wa kuwafundisha wanawake ili waweze kuwa na uwezo wa kuleta mawazo yenye kuinua kampuni au taasisi mbalimbali kuwa kubwa.

Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema serikali itaendelea kutoa fursa sawa kati ya wanawake na wanaume katika vyombo vya maamuzi ili kuinua uwezo wa wanawake na kuchangia katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati akizindua mpango wa kuwawezesha wanawake ujulikanao kama Female Future Tanzania ulioandaliwa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Mhe. Suluhu amesema endapo wanawake watashirikisha katika nafasi za uongozi, bodi za kampuni itaongeza kiwango na chachu ya utendaji nchini.Kwa upande wake Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Vijana Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama amekitaka Chama cha Waajiri Tanzania kiandae mpango utakaowawezesha wasichana wanaohitimu vyuo vya elimu ya juu nchini ili kujikwamua na changamoto ya ukosefu wa ajira nchini.

Mpango huo uliozinduliwa leo umefanywa wanachana chama cha  waajili Tanzania ambao unalenga kuwajengea uwezo wanawake ili kuongeza ufanisi katika biashara zao na kujenga mtandao ambao utaongeza juhudi na maarifa kwa wanawake.

Post a Comment

0 Comments