Business

header ads

WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI YAFUTA VYAMA VYA KIJAMII 1,268 Msemaji wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga akizungumza na waandishi wa habari leo juu ya ufutaji wa vyama vya kijamii vilivyoshindwa kuendesha pamoja na kushindwa kulipa ada, kushoto ni Mwanasheria wa wizara hiyo, Berious Nyasembwa.
Waandishi wa habari wakifatilia taarifa ya Msemaji wa Wizara Mambo ya Ndani ya Nchi, Isaac Nantanga leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.


Na Zainabu Hamisi, Globu ya Jamii.

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imefuta vyama vya Kijamii 1,268 kutokana na kushindwa kutekeleza majukumu yao na sheria zilizowekwa katika uendeshaji wa vyama pamoja na mashirika yasiyo ya Kiserikali (NG’0s).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Isaac Nantanga amesema kuwa kufutwa kwa vyama hivyo ni kutokana na kukiuka masharti ya uwendeshaji wa taasisi ikiwemo kutolipa ada kwa mujibu wa sheria.

Katika ufutwaji wa vyama hivyo chama kimojawapo kilichofutwa ni chama cha wapiga picha nchini ambacho kimeshindwa kukidhi vigezo vya uendeshaji na kushindwa hata kuendesha vikao vyake.

Nantanga amesema kuwa vyama vingine 1,406 vimepewa kusudio la kufutwa na baada siku 21 kuanzia leo, kama havitatoa kusudio la kujitetea basi navyo vitafutwa.

Amesema kufuatana na kanuni ya vyama inayoundwa na kifungu cha 38 cha sheria ya vyama vyote vya kijamii vinapaswa kulipa ada ya kila mwaka.

Aidha, amesema kanuni ya 6 za vyama za kijamii inayosomwa pamoja na kifungu cha 22 cha sheria ya vyama inavitaka vyama vya kijamii kuwasilisha taarifa za kila mwaka za hesabu zilizokaguliwa za mapato na matumizi ya vyama kwa msajili wa vyama.

Aliongeza kuwa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi inatoa angalizo kwa vyama vyote vya kijamii kuendesha shughuli zake kwa kufuatana na sheria zilizoanzisha vyama hivyo.


Post a Comment

0 Comments