Business

header ads

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, VIONGOZI WA JUU WAAFANYA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA AFANYA USAFI JIJINI DAR ES SALAAM

 HAPA KAZI TU ya  Rais wa Jamhuri ya Tanzania Dkt. John Pombe  Joseph Magufuli  ikiendelea kufanyiwa kazi kama Rais  huyo akionekana katika picha akiwa sambamba na mkewe Mama Janeth Magufuli,wakishiriki kufanya usafi leo ndani na nje viunga vya Ikulu ikiwemo pia soko la Samaki Feri,ambako alipata wasaa kuwasikiliza wachuuzi wa samaki na wavuvi.
guf1 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa pamoja na Mama Janeth Magufuli wakielekea eneo la ufukwe wa Ferry kufanya usafi katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru tarehe 9 Desemba.
 

guf3 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizoa taka katika eneo la ferry jijini Dar es Salaam.
guf7 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiweka taka ndani ya ndoo ya Taka katika eneo la Magogoni jijini Dar es Salaam.
guf8 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiwa pamoja na Mke wake Mama Janeth Magufuli wakifanya usafi katika eneo la ufukwe wa ferry jijini Dar es Salaam.
>MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA SULUHU HASSAN ASHIRIKI NA WANANCHI WA ENEO LAKE KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA, MAADHIMISHO YA SIKU YA UHURU.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wakazi wa eneo lake la Oysterbay- Karume Raod, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiingia kukagua eneo la kuhifadhia Taka lililopo eneo la Kituo cha Daladala cha Morocco, wakati alipofika eneo hilo kwa ajili ya kuendelea kushiriki na wananchi kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Mhe. Samia Suluhu Hassan, akishiriki kuzoa taka na baadhi ya wananchi wa eneo Morocco, wakati wa zoezi la kufanya usafi wa mazingira ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania kama alivyoagiza Mhe Rais Dkt. John Pombe Magufuli, ambapo zoezi hilo limefanyika nchini kote hii leo.
***********
WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA USAFI SOKO KUU LA KARIAKOO

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisafisha mtaro wa maji machafu kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akitoka eneo la shimoni kwenye soko kuu la Kariakoo kufanya usafi Desemba 9, 2015. Kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na umati ulioshiriki katika kufanya usafi kwenye soko kuu la Kariakoo jijini Dar es salaam Desemba 9, 2015. Kushoto kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ilala, Raymond Mushi.
(Pichana Ofisi ya Waziri Mkuu)
                               Post a Comment

0 Comments