Business

header ads

MTANGAZAJI WA KITUO CHA TELEVISIHENI CHA EATV AVUNJIWA NYUMBA, AIBIWAWatu wasiofahamika wanaoaminika kuwa ni majambazi wameingia na kuvunja nyumba ya mtangazaji wa kituo cha Television Cha East Africa Television Elikunda Materu eneo la Kinyerezi na kuiba vitu vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tano.

Inasadikika watu hao waliingia nyumbani kwa mtangazaji huyo kuanzia majira ya saa mbili kamili usiku wakati mtangazaji huo bado akiwa kazini katika shughuli za utangazaji.

Akizungumzia tukio hilo Materu amesema alifika nyumbani kwake majira ya saa nne usiku akitokea kazini na ndipo alipokuta grili na mlango ipo wazi na alivyoingia ndani alibaini kuwepo na wizi.

Baaada ya kutokukuta baadhi ya vitu ikiwemo Tv Samsung Flat screen, King'amuzi cha Startimes, majambazi hao walivunja mlango wa chumbani kwake na kufanikiwa kuiba laptop 1 aina ya Dell, Tape recorder aina ya Zoom H2N, Sub Ufa aina ya Sean Piano na Fedha Taslimu sh 250,000.

Kwa yeyote atakayepata taarifa kuhusu uuzwaji wa laptop au simu tafadhali wasiliana nae kwa namba 0717396064 au 0758131487

Post a Comment

0 Comments