Business

header ads

WANAOUZA NGONO WAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWIMwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho  akizungumza na waandishi wa Habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani mwaka huu ambayo inaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi  kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo. 
 Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa TACAIDS Dkt. Jerome Kamwela akiwaonesha waandishi wa Habari Bango lenye Takwimu za Hali ya Maambukizi ya VVU nchini Tanzania.
Kundi la wakina dada wanaouza ngono Jijini Dar es Salaam limetajwa kuongoza

kwa kuwa na maambukizi mengi ya virusi vya Ukimwi kwa kiasi cha asilimia 26 likifuatiwa na kundi la wanaume wanaofanya ngono kwa jinsia moja lenye  asilimia 22, huku kundi la vijana wanaotumia madawa ya kulevya kwa kujidunga sindano likishika nafasi ya tatu kwa kuwa na asilimia 15 yamaambukizi ya Ukimwi.

Takwimu hizo zimetolewa leo Jijini Dar es Salaama ambapo Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Fatma Mrisho amesema licha ya kuwepo kwa makundi hayo yanayoongoza kwa maambukizi ya virusi vya Ukimwi, pia wanaume wamekuwa ni changamoto katika kujitokeza kupima virusi vya Ukimwi na Ukimwi tofauti na wanawake.

Dkt. Fatma Mrisho amesema kupitia maadhimisho ya siku ya Ukimwi duniani kwa mwaka huu watayatumia kuwahamasisha wanaume kujitokeza kwa wingi kupima afya zao ikiwemo virusi vya Ukimwi kwa lengo la kuwalinda wake zao dhidi ya maambukizi mapya ya Ukimwi.WITO umetolewa kwa wananchi kote nchini kuyatumia maadhimisho ya Siku ya UKIMWI duniani ambayo huadhimishwa kila ifikapo Desemba 1 ya kila mwaka kupima afya zao ili kudhibiti maambukizi mapya ya VVU.

Akizungumza na waandishi wa Habari leo jijini Dar es salaam Mwenyekiti Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI nchini Tanzania Dkt. Fatma Mrisho amesema  Siku ya Ukimwi Duniani nchini itaadhimishwa kwa  kuwahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupima afya zao na kupata elimu ya kujikinga  na maambukizi ya ugonjwa huo.

Ameeleza kuwa  maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na shughuli mbalimbali zikiwemo za Utoaji wa Elimu ya Afya na Upimaji wa hiari wa VVU katika maeneo mbalimbali kote nchini kupitia vituo vitakavyowekwa, Kufungua kituo cha maarifa cha udhibiti UKIMWI eneo la Manyoni mkoani Singida ambayo ni njia kuu kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa na nchi za Jirani za Burundi na Rwanda.


Post a Comment

0 Comments