Business

header ads

MAGUFULI AAPISHWA KUWA RAIS WA AWAMU YA TANO WA TANZANIA LEO JIJINI DARRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua gwaride maalum la Jeshi la Ulinzi lenye Umbo la Alfa, ikiwa ni ishara ya kuanza kwa Serikali mpya ya awamu ya tano, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo. Sherehe hizo zimehudhuliwa na viongozi mbali mbali wa ndani na nje ya nchi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akila kiapo mbele ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mh. Mohamed Chande Othman, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.Kushoto ni Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Makamu wake, Mh. Dkt. Mohamed Gharib Bilal. Wa pili kulia ni Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini, Jenerali Davies Mwamunyange, wakati akiwaaga wananchi mara tu alipowasili kwenye Uwanja wa Taifa, katika Sherehe za kuapishwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli, zilizofanyika leo jijini Dar es salaam.
Rais aliemaliza muda wake, Mh. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea salamu ya heshima ya kijeshi kabla ya kukabidhi madaraka kwa Rais Mpya wa awamu ya tano, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli.
Rais Mpya wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Dkt. John Pombe Magufuli akionyesha Mkuki na Ngao aliokabidhiwa na Wazee wa kimila ikiwa ni ishara ya Uongozi wa Kitaifa, katika Sherehe za kuapishwa kwake, zilizofanyika kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam leo.

Rais mpya wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli, ameapishwa rasmi leo kuwa rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Mungano wa Tanzania katika sherehe zilizofana na kuhudhuriwa na maelfu ya Watanzania katika uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.


Akitoa hotuba yake ya kwanza baada ya kuapishwa kuwa rais Dk. Magufuli amewashukuru Watanzania kwa kumchagua kuwa rais wa awamu ya tano na kuwaahidi kuwa atawatumikia bila ya kujali kabila, dini ama itikadi zao za vyama vya siasa.

Dk. Magufuli amesema kuwa uchaguzi mkuu sasa umeisha na rais ni yeye Dk. John Pombe Magufuli, hivyo ameomba kuwepo kwa mshikamano na kuwataka wanasiasa kuweka itikadi zao za vyama kando ili kuwatumikia Watanzania.


Sherehe hizo zilizokamilisha ukomo wa rais wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete zimehudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo rais wa Rwanda Paul Kagame, rais wa Kenya Uhuru Kenyatta, rais Uganda Yoweri Museveni, rais Afrika Kusini Jacob Zuma, Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe, rais Joseph Kabila wa DRC na rais Msumbiji Filipe Nyusi, rais wa Zambia Edger Lungu.

Vile vile pia waliokuwepo kushuhudia sherehe hizo ni pamoja na rais mstaafu wa awamu ya pili Alhaj Ali Hassan Mwinyi, rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa rais aliyemaliza muda wake wa awamu ya nne Dk. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein, rais mstaafu wa Zanzibar Amani Abeid Karume.

Mapema leo wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na viunga vyake walijitokeza kwa wingi katika viwanja vya Uhuru kuhudhuria sherehe hizo ambapo walianza kumiminika katika viwanja hivyo kuanzia saa kumi na mbili asubuhi ili kushuhudia tukio hilo la kihistoria ambapo mvua kubwa iliyonyesha haikuwazuia wanainchi hao kushudia tukio hilo.

Sherehe hizo zilipambwa na gwaride lililoandaliwa na vikosi mbalimbali vya majeshi ya Tanzania, vikiwemo vikosi vya jeshi la anga, maji na ardhini ambavyo vilitoa heshima ya kijeshi ikiwa ni pamoja na ndege za kivita zilizopamba sherehe hizo.

Post a Comment

0 Comments