Business

header ads

JAJI MKUU WA TANZANIA MHE. OTHMAN CHANDE ATOA SOMO KWA WAANDISHI WA HABARIJaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande akitoa ufafanuzi kwa wanabari (hawapo pichani) kuhusu uandishi bora wa habari za Mahakama wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini Dar es salaam.
Rais wa Baraza la Habari Tanzania (MCT) Jaji Mstaafu Thomas Mihayo akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa Habari namna wanavyoweza kuandika habari za Mahakama kwa kuzingatia weledi wa taaluma zao.
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama leo jijini Dar es salaam.
Washiriki wa mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa Habari za Mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Othman Chande leo jijini Dar es salaam.

Na  Aaron Msigwa –MAELEZO.


Vyombo vya habari nchini Tanzania vimetakiwa kuzingatia weledi na kuepuka kuhukumu katika kuripoti habari za mahakamani jambo ambalo limekuwa likiathiri uendeshaji wa kesi mahakamani.

Hayo yameelezwa  jijini Dar es Salaam na Jaji Mkuu wa Tanzania Mohamed Chande Othman wakati wa akifungua semina ya mafunzo ya kuwajengea uwezo waandishi wa habari za mahakama, ambapo amesema kufanya hivyo kutawafanya wananchi kukosa imani na utendaji wa mahakama nchini.

Jaji Mkuu amewataka waandishi kuacha tabia yakuandika habari za mahakama kwa kifupi ambazo zinawaacha wasomaji njia panda bila kupata maelezo kamili ya habari hiyo iliyoandikwa kuhusu shauri fulani.


Post a Comment

0 Comments