Business

header ads

WAKAZI WA JIJI LA MWANZA ,WAELEZA HISIA ZAO KUWA MAGUFULI ANATOSHA NAFASI YA URAIS


 Dkt. Magufuli (katikati) akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Nyamagana (pichani kulia) Ndugu Stanslaus Mabula mbele ya Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo.Baadhi ya wakazi wa jiji la Mwanza waliohojiwa na Globu ya Jamii walieleza na kukiri wazi kuwa haijawahi kutokea kwa mapokezi haya makubwa na ya aina yake,na kuwa Magufuli ndiye anaetosha kuvaa viatu vya Urais.
 Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula 
 Dk Magufuli (katikati) akiwanadi Mgombea Ubunge Jimbo la Ilemela, Anjela Mabula na Stanslaus Mabula ambaye anagombea ubunge Jimbo la Nyamagana.
 Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake wakiwa wamekusanyika mithili ya Utitiri kwenye uwanja wa Furahisha jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifikakapo Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akihutubia  Maelfu ya wakazi wa jiji la Mwanza na vitongoji vyake katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo jijini Mwanza kwenye mkutano wa kampeni,ambapo Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha Mapinduzi CCM,Dkt John Pombe Magufuli aliwahutubia na kuwaomba wampigie kura za kutosha ifika Oktoba 25 kwenye uchaguzi mkuu wa Mwaka huu.
 Sehemu ya umati wa wakazi wa jiji la Mwanza wakishangilia jambo wakati Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alipokuwa akizinadi sera zake. 
 sehemu ya umati wa watu ndani ya viwanja vya furaisha jijini Mwanza jioni ya leo.

 Wananchi wakiuzuia msafara wa Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Pombe Magufuli  uliokuwa ukisindikizwa na umati wa watu kutoka Uwanja wa Ndege wa Mwanza kwenda kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza.

 Wananchi wa Jiji la Mwanza wakiwa wametandika vitenge kwenye lami ili msafara wa Dk Magufuli upite kuelekea kwenye mkutano wa Kampeni katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo jijini Mwanza.
 Mgombea urai wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa kampeni katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza
 Mgombea urai wa Tanzania kupitia CCM, Dk John Magufuli akiwapungia mkono wananchi alipokuwa akiwaaga baada ya mkutano wa kampeni kumalizika katika viwanja vya Furahisha, jijini Mwanza
 Msafara wa Mgombea Urais wa CCM Dkt John pombe Magufuli ukiondoka katika viwanja vya Furahisha jioni ya leo mara baada kumaliza mkutano wa kampeni,huku ukisindikizwa na umati mkubwa wa watu.

PICHA NA MICHUZI JR-JIJINI MWANZA.

Post a Comment

0 Comments