Business

header ads

Tanzania kuadhimisha siku ya Haki za Binadamu Afrika.


 Makamu Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bw. Idd Ramadhan Mapuri akiwasalimia wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar es Saam.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay akitoa neno la ufunguzi kwa wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar es Saam.
Mkurugenzi wa shirika lisilo la Kiserikali la Help Age Bw. Smart Daniel akiwasilisha mada kwa wazee na watetezi wa haki za binadamu (hawapo pichani) wakati wa semina juu ya haki za wazee mapema hii leo jijini Dar es Saam.
Baadhi ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi juu ya haki za wazee iliyoratibiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Help Age mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi juu ya haki za wazee iliyoratibiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala kwa kushirikiana na shirika lisilo la Kiserikali la Help Age mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazee na watetezi wa haki za binadamu walioshiriki semina elekezi juu ya haki za wazee wakimsikiliza kwa makini Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay wakati akitoa neno la ufunguzi mapema hii leo jijini Dar es Salaam.                                                                                           (Picha zote na Eliphace Marwa)Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Tanzania kwa kushirikiana Shirika lisilo la kiserikali la Help Age Tanzania zinaujulisha umma kwamba tarehe 21 Oktoba 2015 kutakuwa na maadhimisho ya Siku ya Haki za Binadamu Afrika.

Maadhimisho hayo yatakayofanyika katika Hoteli ya New Afrika jijini Dar es Salaam ambapo viongozi mbalimbali wa Serikali na Mabalozi wa Afrika watahudhuria maadhimisho hayo yenye lengo la kulinda na kutetea haki za wazee Tanzania.

Akizungumza na Wazee na watetezi wa haki za binadamu, Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Bi. Mary Massay amesema kuwa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora inawajibika Kitaifa kufuatilia hatua za utekelezaji wa haki za binadamu hususani wazee ili waweze kuishi kwa furaha, amani na usalama kinyume na sasa Ambapo wazee wamekuwa wakiuawa kwa imani za kishirikina.

Maadhimisho haya ya haki za Binadamu Afrika ni sehemu ya Mpango-Kazi wa Kitaifa wa Haki za Binadamu ambao ni mkakati wa Serikali wa miaka mitano (2013 – 2017) wenye lengo la kutoa dira kwa Serikali yenyewe kwa maana ya Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na Asasi za Kiraia na wananchi kwa ujumla jinsi ya kukuza, kulinda na kuhifadhi haki za binadamu ili kuimarisha utawala bora nchini.

Naye Mkurugenzi toka Shirika lisilo la Kiserikali la Help Age Bwana Smart Daniel amesema kuwa kati ya nchi 96 Duniani Tanzania iko katika nafasi ya 92 kwa kulinda haki za wazee kwa kuzingatia vigezo vya upatikanaji wa huduma bora za afy, mazingira wezeshi kwa wazee, uhakika wa kipato kwa wazee pamoja na uwezeshwaji wa wazee katika fursa mbalimbali ili kujipatia kipato.

"Katika suala la kipato Tanzania iko nafasi ya 94 kwa kujali wazee kwa kuwalipa pensheni, katika suala la Afya kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 66 na katika suala la mazingira wezeshi kwa wazee Tanzania iko nafasi ya 88 na hii inatokana na kutokuwepo kwa sheria ya wazee", alisema Bwana Smart.

Aidha, Maadhimisho haya yanalenga kuongeza uelewa kwa umma juu ya wajibu alionao kila mwananchi wa kutetea, kulinda, kuhifadhi na kuhamasisha haki za binadamu nchini ili kudumisha amani, utulivu na maendeleo endelevu.

Post a Comment

0 Comments