Business

header ads

MGOMBEA UBUNGE WA LUDEWA DEO FILIKUNJOMBE ATHIBITISHWA KUFA KATIKA AJALI YA HELKOPTAJerry INSTA
Jerry Silaa amepost Ujumbe huu akithibitisha kufariki kwa Mbunge Deo Filikunjombe pamoja na baba yake, Mzee William Silaa ambaye alikuwa Rubani wa Helikopta hiyo >>> “Kwa masikitiko makubwa nimepokea taarifa rasmi kutoka kwa timu ya uokoaji imefanikiwa kufika eneo la ajali na kukuta abiria wote na rubani wamepoteza maisha…. Nimepoteza Baba na rubani mzuri wa nchi yetu Capt.William Silaa, nimepoteza rafiki na kiongozi wangu Mhe. Deo Filikunjombe. Nawapa pole wote waliopoteza ndugu zao. Nawaombea marehemu mapumziko ya Amanijerrysilaa
Hii ni picha ya zamani, Mbunge Zitto Kabwe akiwa na Marehemu Deo Filikunjombe.
Hii ni picha ya zamani, Zitto Kabwe akiwa na Marehemu Deo Filikunjombe.
Nawashukuru wote walioshirikiana na familia kusaidia uokozi. Namshukuru Mhe.Rais Jakaya M Kikwete, Dr.John Pombe Magufuli, IGP Ernest Mangu, Katibu Mkuu MU Dr. Meru, Kampuni ya Everest Aviation ,Wabunge, MaDC, Maafisa wa TCAA na wote walioshiriki kuwatafuta wahanga wa tukio hili. Tutajuzana taarifa na mipango mingine. JS jerrysilaa
Deo Filikuonjome
Marehemu Deo Filikunjombe na baadhi ya Wapigakura wake wa Jimbo la Ludewa, Mkoa wa Njombe.
HABARI YA UHAKIKA
Aliyekuwa mgombea ubunge wa jimbo la Ludewa kupitia tiketi ya chama cha mapinduzi CCM Deo Filikunjombe na wengine watatu wamefariki dunia katika ajali ya helkopta iliyotokea jana eneo la hifadhi ya Selous.


Akidhibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi Paul Chagonja amesema ndege hiyo ilikuwa imebeba abiria wanne wakitokea Dar es salaam kuelekea Njombe na kuwa waliotambuliwa mpaka sasa ni rubani wa ndege hiyo Kapteni William Silaa na Deo Filikunjombe.


Kamishna Chagonja amesema mpaka sasa uchunguzi wa ajali ya ndege hiyo yenye namba za usajili 5Y- DKK unaendelea na kuwa abiria wengine wawili bado hawajatambulika majina yao

Post a Comment

0 Comments