Business

header ads

Mahakama yatoa uamuzi kuwa hakuna mtu anayetakiwa kukaa umbali zaidi ya mita 200

 Wakili aliyekuwa anasimamia kesi upande wa mpiga Kura Peter Kibatala akizungumzia hatma ya kesi hiyo na dhamira ya kukata rufaa

 Naibu Mwanasheria mkuu wa serikali Dkt. Tulia Akson akijibu maswali ya waandishi
Mahakama Kuu ya Tanzania leo imetoa uamuzi wa kesi lililofunguliwa kwa hati ya haraka likitaka tafsiri ya sheria ya uchaguzi ya  kifungu namba 104 (1) kuhusu umbali wa mita 200 ambao mpiga kura anastahili kukaa kwa utulivu akisubiri matokeo na kusema kuwa haruhusiwi mtu yeyote kukaa hata kwenye umbali zaidi ya mita hizo.

Akisoma Hukumu ya kesi hiyo nambari 37 ya mwaka 2015 Jaji Jaji Lugano Mwandambo kwa niaba ya Majaji wenzake wawili Jaji Sekieti Kihiyo na Jaji Aloycius Mujulizi amesema baada ya kusikiliza hoja za mawakili wa pande zote mbili Mahakama imesisitiza makatazo yote yaliyo katika kifungu namba 104 katika sheria hiyo na kuainisha kuwa wapiga kura hawaruhusiwi kukaa katika eneo hilo.

Jaji Mwandambo amesema kwa kuwa kifungu hicho cha sheria ya sheria ya uchaguzi namba 343 iliyofanyiwa Marekebisho mwaka 2010, kinaelezea bayana kuhusu kukaa au kukusanyika katika eneo la kupigia kura.

Kesi hiyo ilifunguliwa  kwa hati ya haraka na mpiga kura Amy Kibatala ambaye anaitaka Mahakama Kuu nchini Tanzania kutoa tafsiri  ya sheria ya uchaguzi ya  kifungu namba 104 (1) kuhusu umbali ambao mpiga kura anastahili kukaa kwa utulivu akisubiri matokeo, mlalamikaji alikuwa anawakilishwa na wakili Peter Kibatala.

Post a Comment

0 Comments