Business

header ads

WATANO WAFARIKI KWA KIPINDUPINDU, KINONDONI


Idadi ya vifo vililivyosababishwa na ugonjwa wa kipindupindu katika Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imeongezeka na kufikia watano baada ya hii leo watoto wawili kufariki dunia kwa ugonjwa huo.

Akiongea leo jijini Dar es Salaam, Mganga Mkuu wa Manispaa ya Kinondoni Dkt. Azizi Msuya amesema kuwa idadi ya wagonjwa imeendelea kuongezeka kutoka 52 hapo jana na kufikia 58 kutokana na wananchi kutozingatia maagizo wanayopewa na madaktari ili kuhakikisha ugonjwa haoauendelei kuwaambukiza watu wengine.
Aidha, Dkt. Aziz amesema wagonjwa wanaongezeka wanatoka katika maeneo mbalimbali ya wilaya ya Kinondoni ikiwa ni pamoja na maeneo mapya yaliyopata maabukizi na sasa wamefikia wagonjwa zaidi ya 100 waliopokelewa na kutibiwa hadi sasa.

Post a Comment

0 Comments