Business

header ads

RAIS KIKWETE AKIONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU DODOMAKatibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akipanga nyaraka vizuri kwenye meza kuu, kabla ya kikao cha Kamati Kuu ya CCM, kuanza leo, katika Ukumbi uliopo jengo la White House, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma.

Baada ya kikao hicho kuanza Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye alitoka ukumbini na kuwaambia  Waandishi wa Habari kwamba, moja ya maazimio ya Kikao hicho ni kwamba kura za maoni zitarudiwa keshokutwa Alhamisi, katika majimbo matano ya Ukonga, Kilolo, Busega, Rufiji na Makete  ambako yamejitokeza malalamiko na kufika katika vikao vya Chama, kuhusiana na kura za maoni za awali
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwasili katika ukumbi uliopo jengo la White House, Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma, kuendesha Kikao cha Kamati Kuu ya CCM leo mjini Dodoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya CCM, leo Agosti, 11, 2015 katika ukumbi wa Jengo la White House Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Philip Mangula na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimkaribisha Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuzungua kikao hicho. Kushoto  ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohammed Shein na kulia ni Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula
Kikao cha Kamati Kuu kikiendelea. Post a Comment

0 Comments