Business

header ads

POLISI YAWATAHADHARISHA WANAOFANYA MAKOSA YA MITANDAO

Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia Profesa Makame Mbarawa amesema kuwa sheria mpya ya Makosa ya Mitandao itakayoanza kutumika tarehe 1 mwezi ujao hailengi kikundi fulani cha watu ila watanzania wote.

Profesa Mbarawa ameyasema hayo katika mkutano wa pamoja na Makamanda wa Jeshi la Polisi ulioitishwa ili kuwajengea uwezo Makamanda kuifahamu vizuri sheria hiyo kabla ya kuanza kutumika rasmi.

Naye Kamishani wa Polisi kitengo cha Polisi jamii aliyemwakilisha Mkuu wa Jeshi la Polisi, Kamishina Musa Ali Musa amewataka wananchi kuisoma vizuri sheria hiyo ili waijuwe na kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao kama matusi, picha chafu na wizi katika mabenki ambapo kabla ya sheria hii watu walikuwa wakifanya makosa ila kwa kukosekana sheria jeshi la polisi lilikosa nguvu za kisheria kuwakamata wahalifu wao wa mitandaoni............

Post a Comment

0 Comments