Business

header ads

PATO LA TANZANI LAONGEZEKA

Pato la Taifa nchini Tanzania—GDP limeongezeka kutoka wastani wa shilingi trilioni kumi na nane zilizopatikana mwaka jana na kufikia shilingi trilioni 21.9 katika robo ya kwanza ya mwaka huu, huku mchango wa baadhi ya sekta katika uchumi ikiwemo ile ya madini ukiwa umeporomoka.

Mkurugenzi wa Takwimu za Kiuchumi kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu Bw. Morris Oyuke, amesema hayo leo na kwamba pato hilo limeongezeka licha ya kasi ya ukuaji wa uchumi nayo kupungua kutoka ukuaji wa asilimia nane nukta sita hadi asilimia sita nukta tano

 Kwa mujibu wa Oyuke, mafanikio hayo yanaifanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza katika ukanda wa Afrika Mashariki kwa ukuaji mzuri wa uchumi na pato la taifa, ikifuatiwa na nchi ya Kenya huku Burundi ikishika nafasi ya mwisho

Post a Comment

0 Comments