Business

header ads

NEC YAPOKEA FOMU ZA WAGOMBEA WA URAISMwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akimkabidhi, Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, nyaraka mbalimbali zitakazotumika wakati wa Kampeni za Uchaguzi Mkuu, kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam leo Agosti 21, 2015. Kushoto ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji Damian Lubuva akizungumza mara baada ya kupokea Fomu zilizorudishwa na Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa na Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni baada ya kukamilisha mchakato wa kutafuta wadhamini katika Mikoa 10 ya Tanzania na kutimiza masharti yote ya Uchaguzi, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam.Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe akifatiwa na Katibu Mkuu wa CUF na Mgombea Urais wa Zanzibar wa UKAWA kupitia Chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad.
Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutangazwa rasmi na Tume ya Uchaguzi kuwania nafasi hiyo, leo Agosti 21, 2015 kwenye Ofisi za Tume hiyo, Jijini Dar es salaam. Pembeni yake ni Mgombea Mweza wake, Dkt. Juma Haji Duni

HABARI KAMILI

Tume ya Taifa ya Uchaguzi nchini Tanzania (NEC) imemtangaza Mhe. Edward Ngoyai Lowassa kuwa mgombea urais kupitia chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na Mhe. John Pombe Magufuli kuwa mgombea urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM, baada ya kutimiza vigezo vya kugombea urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.

Wagombea wengine waliorudisha fomu za kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika uchaguzi mkuu utakaofanyika tarehe 25 Oktoba ni pamoja na Machmilian Lyimo wa TLP, Chief Lutalosa Yemba wa (ADC) na Hashim Rungwe Spunda wa (CHAUMA).

Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, maara baada ya kuzipokea fomu za wagombea hao Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva amewataka wagombea hao wafuate kanuni na maadili ya uchaguzi, huku wakikabidhiwa nyaraka sita ikiwa ni pamoja na katiba ya Tanzania, waraka wa kufuata kanuni na maadili pamoja na kanuni cha uchaguzi.


Post a Comment

0 Comments