Business

header ads

JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU MAANDAMANO WAKATI WA KUCHUKUA FOMO TUME YA UCHAGUZI

Jeshi la Polisi nchini Tanzania leo limeamuru kusitishwa kwa maandamano ya aina yoyote wakati wote wa zoezi la kuchukua fomu kutafuta wadhamini mikoani na hata wakati wa kurejesha fomu kwa wagombea wa nafasi mbali mbali.Naibu Inspekta Jenerali wa Jeshi la Polisi Abdulrahman Kaniki ametoa agizo hilo leo wakati akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya jeshi hilo jijini Dar es Salaam katika kile alichokielezea kuweka hali ambayo haitaleta usumbufu au kuhatarisha usalama wa raia na mali zao.

Aidha, Kaniki amesema kuwa unafanyika utaratibu wa kuwakutanisha wadau wote wa siasa ikiwa ni pamoja na viongozi wote wa vyama vya siasa kufanya majadiliano ya namna ya kuhakikisha kwamba mchakato mzima wa uchaguzi unafanyika katika hali ya amani na utulivu.

Post a Comment

0 Comments