Business

header ads

IDADI YA WANUFAIKA WA MIKOPO ELIMU YA JUU YAONGEZEKAKaimu Mkurugenzi Habari, Elimu na Mawasiliano Bw. Cosmas Mwaisobwa akiongea na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu
kuongezeka kwa Idadi ya wanafunzi    wanaopata  mikopo kutoka   Bodi ya Mikopo  ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) ambapo kwa  mwaka 2005/2006 wanafunzi 42,729  walipata mkopo na mwaka  2014/2015 wanafunzi  98,000 walinufaika.
 (picha na Frank Mvungi) 

Na Jenikisa Ndile

Idadi ya wanafunzi    wanaopata  mikopo kutoka   Bodi ya Mikopo  ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imeongezeka mwaka hadi mwaka kutoka wanafunzi 42,729 mwaka 2005/2006 hadi kufikia wanafunzi  98,000 kwa mwaka  2014/2015.

Sambamba na hilo   kiasi  cha fedha  kilichotolewa na bodi kwa ajili ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu  nacho kimeongezeka kutoka  sh.  bilioni 56.1  hadi kufikia  sh. bilioni 345 katika kipindi hicho.

Hayo yalisemwa leo Jijini Dar es Salaam na Kaimu Mkurugenzi  wa Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka bodi hiyo Cosmas wakati akizungumza na waandishi wa  habari kwenye ukumbi wa mikutano wa Idara ya Habari (MAELEZO) kuhusu mafanikio ya  bodi hiyo katika kipindi hicho.

Alisema kwa kipindi hicho chote  wamekuwa na sheria mbalimbali ilioanzishwa kwa kuwapa jukumu la ukusanyaji wa madeni ya mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu ambayo ilianza kutolewa tangu mwaka 1994/1995 kupitia iliyokuwa Wizara ya Elimu,Sayansi na Teknolojia wakati huo Serikali haikukusanya madeni kutoka kwa wanufaika hadi pale bodi  ilipoanza kazi rasmi mwaka 2006/2007.

Aliongeza kuwa taasisi hiyo imekuwa  na mafanikio makubwa kulinganisha na hapo awali kwani kwa kipindi cha miaka kumi tumeongeza ufanisi katika matumizi ya teknolojia  ya habari na mawasiliano (TEHAMA)  kwa lengo la kuomba mikopo kwa njia ya mtanda kupitia mfumo wa uombaji wa mikopo wa tovuti.

Aidha  bodi hiyo  imeendelea kukua kwa kasi kutokana na idadi ya watumishi kutoka tisa hadi kufikia watumishi 135 mwaka huu,ongezeko hilo limesaidia bodi kuwa na ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake.

Bodi hiyo imewawezesha wateja wake  kupata huduma katika maeneo manne ambayo ni  Arusha, Mwanza, Dodoma, na Zanzibar ili kupata huduma za kibodi kwa ukaribu zaidi.

Mwaisongwa   aliwahakikishia wateja  hao  wataendelea kuwanufaisha waombaji na kutambua kuwa mikopo ya wanafunzi  wa elimu ya  juu ni sehemu ya utekelezaji wa sera ya uchangiaji wa elimu ya juu na ni muhimu kurejesha mikopo ili kuwezesha mfuko huo  kuwa endelevu.

Taasisi hiyo iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria namba  9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi julai 2005 yenye lengo la kutoa mikopo kwa wanafunzi i wa elimu ya juu,utoaji na ukusanyaji wa mikopo ili kufanya mfuko wa mikopo kuwa endelevu.
 

Post a Comment

0 Comments