Business

header ads

DKT. MENGI KUANZISHA KAMPUNI YA KUSAIDIA VIJANA

Mwenyekiti Mtendaji wa Makampuni ya IPP Dkt. Reginald Mengi amesema hivi karibuni ataanzisha shindano jipya la vijana kutoka nchi za Afrika Mashariki lenye lengo la kubuni wazo jipya la kibiashara na kuwataka vijana wa Tanzania kuelewa kwamba shindano hilo sasa litakuwa na ushindani mkubwa hivyo wanachopaswa kufanya ni kujiamini.


Dkt. Mengi amesema hayo leo Jijini Dar es Salaam wakati alipokuwa akikabidhi zawadi kwa washindi kumi wa shindano kutwiti la kubuni wazo jipya la kibiashara kwa mwezi Juni ambapo mshindi wa kwanza alikuwa ni God Ngarumia kutoka Mwanza

Aidha Dkt. Mengi amewataka vijana hao kuhakikisha wanatumia mitandao ya kijamii katika kutangaza biashara zao wanazozifanya ili watanzania wengi zaidi waweze kufahamu na kutambua umuhimu wa kushiriki shindano hilo

Katika hatua nyingine Dkt. Mengi amesema ataanzisha kampuni ambayo itashiriki kwa asilimia 20 katika kusaidia vijana walioweza kuanzisha kampuni zao mara baada ya kushinda katika shindano hilo...

Post a Comment

0 Comments