Business

header ads

RAIS KIKWETE AONGOZA KIKAO CHA KAMATI KUU YA CCM MJINI DODOMA LEO, TANO BORA YA WAGOMBEA KUPATIKANA BAADA YA KIKAO HIKIMwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM, Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza Kikao cha Kamati Kuu ya CCM (CC) kinachoendelea hivi sasa kwenye Ukumbi wa White House, Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma. Kikao hiki kinapitia majina yote 38 ya Watangaza nia ya kugombea Urais kwa tiketi ya CCM, ambapo majina matano yatapatikana baada ya kikao hiki.Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM - Zanzibar, Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dkt. Ali Mohamed Shein, Makamu Mwenyekiti wa CCM - Bara, Mzee Phillip Mangula (kulia) pamoja na Katibu Mkuu wa CCM, Ndg. Abdulrahman Kinana.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, DODOMA.
Sehemu ya Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM wakiwa kwenye Kikao cha kupitia Wagombea wanaowania nafasi ya Urais wa Tanzania kupitia CCM, ambapo majina matano yatapatikana katika kikao hiki na kupelekwa kwenye Mkutano wa Halmashauri kuu ya CCM ili kupata majina matatu yatakayokwenda kupigiwa kura kwenye Mkutano Mkuu.
Baadhi ya Wapigapicha za Habari wakichukua taswira ya Wazee wa Kamati ya Ushauri wa Chama.
Wazee wa Kamati ya Ushauri ya CCM ikiongozwa na Rais Mstaafu awamu ya Pili, Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais Mstaafu awamu ya tatu, Mh. Benjamin Mkapa, Makamu Mwenyekiti mstaafu wa CCM, Mzee Pius Msekwa, Rais Mstaafu wa Zanzibar, Mh. Aman Abeid Karume, Waziri Mkuu Mstaafu, Mh. Cleopa Msuya pamoja na Waziri Mkuu Mstaafu, Dkt. Salim Ahmed Salim.


Post a Comment

0 Comments