Business

header ads

NEC YASOGEZA UANDIKISHAJI DAR ES SALAAM


JAJI DAMIAN LUBUVA
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesogeza mbele zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura katika jiji la Dar es salaam mpaka Julai 22 mwaka huu kutoka julai 16,iliyopangwa hapo awali

Kwa Mujibu Mwenyekiti wa NEC, Jaji Mstaafu Damian Lubuva uamuzi huo umefikiwa baada ya kuridhia maombi ya wadau wa uchaguzi kutaka kusogezwa mbele siku ya kuanza zoezi hilo ili kutoa fursa kwa wananchi kusherehekea Siku Kuu ya Eid-El-Fitri.

Katika taarifa yake Jaji Mstaafu Lubuva amesema wamezingatia kwa uzito maombi hayo ya wadau wa uchaguzi na sasa wamesogeza mbele tarehe ya kuanza kwa zoezi la uandikishaji jijini Dar es Salaam mpaka Julai 22 na kumalizika Julai 31 mwaka huu
Post a Comment

0 Comments