Business

header ads

KITUO CHA POLISI BUNJU CHACHOMWA MOTO.Baadhi ya Polisi wakiwatawanya watu (hawapo pichani) kwa mabomu ya machozi mara baada ya tukio la kuchomwa moto kituo cha polisi Bunju, tukio hilo limetokea.Kituo cha polisi Bunju kilichopo nje kidogo ya jiji la Dar kimechomwa moto na baadhi ya Wananchi kufuatia tukio la kudaiwa kwa Mwanafunzi mmoja kugongwa na gari na kufa papo hapo.
 Sehemu ya kituo hicho cha Polisi Bunju kikiteketea kwa moto mara baada ya kuchomwa moto na wananchi kufuatia tukio la kudaiwa kwa Mwanafunzi mmoja kugongwa na gari na kufariki papo hapo.
 Muonekano wa kituo hicho cha Polisi Bunju mara baada ya kuchomwa moto.
 Moja ya Gari iliyokuwepo kituoni hapo ikiwa imenyofolewa vifaa vyake wakati wa vurugu hizo
 Mmoja wa askari akikagua uharibifu mkubwa uliofanywa katika gari hilo kufuatia vurugu za kuchomwa moto kituo hicho cha Polisi Bunju mapema leo na wananchi.
 Imevunjwa kioo chote cha nyuma
Baadhi ya polisi wakiangalia uharibifu uliofaywa na baadhi ya watu waliovamia kituo  hicho cha polisi Bunju,kufuatia tukio la kudaiwa kugongwa na gari mwanafunzi mmoja na kufa papo hapo.

Baadhi ya wakazi wa Bunju wamevamia na kukichoma moto kituo cha polisi Bunju A baada ya polisi kufyatua mabomu ya machozi na risasi za moto kuwatawanya wananchi waliofunga barabara baada ya kugongwa na gari mwanafunzi na kufa.

Polisi walilazimika kukimbia na gari lao baada ya kuona wananchi wanawazidi nguvu kwa kurusha mawe na kukiacha kituo hicho bila ya ulinzi ndipo wananchi walipokivamia kituo kuvunja milango na kuwatoa wahalifu waliokuwa wakishikiliwa na kisha kukichoma moto.

Awali leo asubuhi gari lilimgonga mwanafunzi wa darasa la nne wa shule ya Msingi Bunju A, na kufa papo hapo na kisha dereva wa gari hilo kukimbia, jambo lililoamsha hasira za wananchi na kufunga barabara kudai matuta.Post a Comment

0 Comments