Business

header ads

HUKUMU YA YONA,MRAMBA YAARISHWA HADI JULAI 6

HUKUMU ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona, imeahirishwa tena katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo hadi Jumatatu ya Julai 6, mwaka huu saa 7 mchana.
Kesi hiyo imeahirishwa baada ya mmoja wa jopo la mahakimu wanaosikiliza kesi hiyo kuwa mgonjwa na kwa ushauri wa daktari ni kwamba anahitaji mapumziko. Hivyo hukumu hiyo itasomwa Jumatatu ijayo.
Akitoa taarifa hiyo, Hakimu Saul Kinemela ambaye ni mmoja wa jopo la mahakimu watatu wanaosikiliza kesi hiyo, amesema mwenyekiti wa jopo lao ambaye ni Jaji John Utamwa ni mgonjwa na kwa ushauri wa daktari hasingeweza kuhudhuria mahakamani hapo. 
Watuhumiwa hao wanakabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya shilingi bilioni 11.7.

Post a Comment

0 Comments