Business

header ads

WAUZA MBAO HARAMU WAONYWASerikali za Tanzania na Zambia leo zimesaini makubaliano yatakayoziwezesha nchi hizo kuzuia biashara haramu ya mbao na mazao ya misitu, inayovunwa kimagendo katika misitu iliyo mpakani mwa nchi hizo mbili.

Waziri wa Maliasili na Utalii wa Tanzania, mheshimiwa Lazaro Nyalandu, amesaini makubaliano hayo kwa niaba ya Tanzania wakati kwa upande wa Zambia, makubaliano hayo yamesainiwa na Waziri wa ardhi, maliasili na ulinzi wa mazingira wa nchi hiyo Bi. Christabel Ngimbu.

Waziri Nyalandu amesema kuwa makubaliano hayo yatatoa fursa ya ulinzi na uvunaji sahihi wa maliasili za misitu, hususani miti ya miombo ambayo imekuwa ikitumiwa kwa mbao ambazo majangili huzivuna kiholela kutokana na mwanya wa ukosefu wa ulinzi wa uhakika katika eneo hilo..

Post a Comment

0 Comments