Business

header ads

VIJANA WAUZA NAFASI ZA KUJIANDIKISHA KWA MFUMO WA BVR

Zoezi la uandikishwaji wapiga kura kwa njia ya mfumo mpya wa kielektronik wa BVR mkoani Arusha, limeingia katika sura mpya ambapo baadhi ya wananchi waandikishwaji kuuza nafasi zao kwa kati ya shilingi 25,000 hadi 30,000.

Mmoja wa vijana hao Hamisi Juma wa kituo cha Muriet Sekondari Kata ya Sokon One, ameuza nafasi yake kwa Neema John kwa shilingi 30,000 kwa madai ya kupata kipato na kufidia siku yake aliyopoteza tangu usiku wa saa nane alipofika kituoni hapo kujipanga hadi muda wa saa sita mchana bila kupata kitambulisho.

Amesema kuliko arudi nyumbani bila mboga ya watoto kwa kupoteza siku, bora auze apate fedha za kutumia na kesho yake atakayokuja ajipange kwa amani.

Nae Lameck Sekeyan wa kituo cha Ebenezer, Kata ya Muriet, amesema yeye ameuza nafasi yake kwa mtu mwingine kwa shilingi 25,000, kwa sababu yeye ni kijana anaweza kurudi kesho kujipanga upya na kupata kitambulisho.

Post a Comment

0 Comments