Business

header ads

PROF JAY SITOACHA MUZIKI KWA SABABU YA SIASA

Rapper Joseph “Professor Jay” Haule, amewaondoa hofu mashabiki wake kuwa hata akifanikiwa kuchaguliwa na kuingia bungeni hatauweka pembeni muziki.
profesa-Jay
“Iwapo wana Mikumi hawatanipa ridhaa ya kuendelea kuwatumikia basi nitaendelea na kazi yangu ya muziki ambayo nimekuwa nikiifanya kila siku.” Prof. Jay ameiambia E-Newz ya EATV. “ Nimekuwa nikiwaambia mashabiki wangu hata nikiingia mjengoni na kwenda kuwatumikia wana Mikumi sitaacha sanaa kwasababu nimekulia sanaa, naishi sanaa na nitakufa ndani ya sanaa.”
“Kwahiyo hata nikiwa mjengoni nitaendelea kuitumikia sanaa na nitaendelea kufanya muziki kama kawaida kama ambavyo wabunge wengine wanaendelea kufanya, sababu mule kuna madaktari kuna wainjilisti lakini wakimaliza shughuli za bunge wanarudi kuendelea na shughuli zao. “ Alimaliza.
SC BONGO 5

Post a Comment

0 Comments