Business

header ads

NEC KUSHUGHULIKIA WANAOSABABISHA VURUGUTume ya Taifa ya Uchaguzi NEC imesema kwamba inaendelea na zoezi la kuwashughulikia kisheria wale wote wanaosababisha fujo na vurugu kwenye vituo vya uandikishaji wapiga kura kwa mfumo wa BVR na kuhatarisha usalama wa watanzania ili wananchi waweze kujiandikisha bila hofu yoyote.

Mwenyekiti wa tume hiyo Jaji Mstaafu Damiani Lubuva ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipohojiwa na East Africa Radio kuhusu hali ya sitofahamu kiusalama iliyojitokeza katika baadhi ya vituo vya uandikishaji wapiga kura katika baadhi ya mikoa ambayo zoezi hilo linaendelea.

Aidha Jaji Mstaafu Lubuva ameongeza kuwa NEC wanashirikiana na Jeshi la Polisi kuhakikisha ulinzi na usalama unaimarika kwenye vituo vya uandikishaji na kuwataka wananchi waaache tabia ya kutembea usiku kwenda kwenye vituo hivyo kwani wanahatarisha maisha yao kufuatia tume kusema endapo muda uliopangwa kuandikishwa utaisha wataongeza muda zaidi.

Jaji Lubuva amewataka wananchi kuendelea kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapigakura kwa mfumo wa BVR nchini ili kutumia haki yao ya kumpata kiongozi wananyemuamini atawaongoza kulingana na malengo yao kitaifa.

Post a Comment

0 Comments